• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kilindi District Council
Kilindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara/Vitengo
      • Idara
        • Elimu Msingi
        • Elimu Sekondari
        • Afya na Ustawi wa Jamii
        • Maendeleo ya Jamii
        • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Ardhi na Maliasili
        • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
        • Usafi na Mazingira
      • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Shughuli za Mifugo na Uvuvi
    • Shughuri za Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji na Umwagiliaji
    • Huduma za Kilimo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu na Majukumu yake
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao vya Kisheria
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Mradi wa Maji
      • Miradi ya Afya
    • Miradi inayoendelea
      • Huduma za Afya
      • Mradi wa Maji
    • Miradi iliyokamilika
      • Huduma za Afya
      • Mradi wa Maji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video Mbalimbali

KIKAO CHA UCHUNGUZI WA TATHMINI YA ATHARI KWA MAZINGIRA NA JAMII WA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA LA AFRIKA MASHARIKI

Posted on: June 2nd, 2017

Mkurugenzi wa kampuni ya JSB ENVI-Dep LTD Bi.Saada Juma wa kwanza kulia katika picha akiwa na Ndg.Mgisha Pastori wa pili kulia na Afisa Usafi na Mazingira  wa wilaya ya Kilindi Ndg.Winston Temba wa kwanza kutoka kushoto wakiwa katika Kikao cha tathmini ya athari za mazingira na jamii zinazoweza kusababishwa na mradi pendekezwa wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi africa mashariki (East africa crude oil pipeline-EACOP), Linalotarajia kupitishwa katika halmashauri ya wilaya ya kilindi.

Tathmini  ya  athari  ya mazingira na jamii zinazoweza kusababishwa na mradi pendekezwa wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi Afrika mashariki unaanzia kutoka kwenye  eneo la ugunduzi lililopo  kusini mwa  ziwa  Albertine nchini Uganda hadi rasi ya chongoleani  iliyopo kasikazini mwa bandari ya Tanga Tanzania kwa ajili ya kusafirisha nje kwenye soko la kimataifa.

Wataalamu elekezi toka kampuni ya JSB Envi-Dep LTD ya kufanya tathmini ya athari ya mazingira na jamii zinazoweza kusababishwa na mradi pendekezwa  walieleza kwakina juu  ya mradi utakavyotekelezwa  hatua kwa hatua kwa wajumbe wa kikao kutoka Ofisi ya Mkuu(W) kilindi ambayo pia ni kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (W) Kilindi, Viongozi wa kata ambazo bomba la mafuta litapitia pamoja na wadau wengine.

Wataalamu wa JSB ENVI-Dep LTD waliwaelekeza wajumbe wa kikao kuwa ukiachana na jinsi mradi utakavyo tekelezwa kuna faida zake pia ambazo ni Kutoa ajira na fursa za biashara kama kutengeneza ajira za muda mfupi (miaka 2-3) na kutoa mafunzo kwa wenyeji, kusaidia mahudhui na manunuzi ya ndani

Pili kushiriki katika programu za maendeleo kama usalama barabarani na kujenga uwezo na Faida ya mwisho ni kuimarisha miundombinu kama vile barabara.

Pia watalaam hao walitoa furusa kwa wajumbe kutoa maoni, kuuliza maswali, mapendekezo na masuala yote yanayohusiana na mradi  ili yaweze kuzingatiwa kwenye mchakato wa tathmini ya athari za mali na kubainisha njia za kupunguza  ili kuhakikisha mradi unaendelezwa bila ya kusababisha athari kwa mazingira ya jamiii.

Watalaam walitaja kata ambazo bomba la mafuta ghafi litapitia kwa wilaya ya Kilindi kuwa ni Kibirashi, Kisangasa,  na Mkindi. Lakini pia walisema pia katika kijiji cha Gitu kilichopo kata ya Kibirashi itajengwa kambi kubwa yenye uwezo wa kubeba wafanyakazi  1000 pamoja na kuhifadhi vifaa kwaajili ya ujenzi  huu.

Aidha watalamu elekezi kutoka  kampuni ya JSB ENVI-DEP LTD waliwataka viongozi ngazi za kata ambao bomba litapitia kubainisha shughuli za maendeleo zinazofanyika kwenye maeneo yao pamoja na vitu vinavyopatikana mfano maeneo ya matambiko, makaburi, misitu ya asili mabwawa n.k, ambapo vitu muhimu vilivyobainishwa ni Maeneo ya Shule, Maeneo ya Madini kama vile Kijiji cha Kinkwembe kilichopo kata ya Mkindi, Mashamba ya Kilimo na malisho ya mifugo, Malambo ya Maji na Bwawa la Maji la Kwamaligwa lililopo kata ya Kibirashi na Misitu ya Hifadhi ya eneo liitwalo Java.

Vingine ni maeneo ya watu binafsi na maeneo ya hifadhi za vijiji na kata.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA KILINDI March 26, 2018
  • TANGAZO LA UHAKIKI WA VYETI VYA WATUMISHI KILINDI March 26, 2018
  • UTOAJI WA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI WA KILINDI April 06, 2018
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkuu wa Wilaya:”Hakikisheni kila kata inapanda miti 93,952”

    April 04, 2018
  • Vikundi vya wanawake Wilayani Kilindi vyapata neema

    March 10, 2018
  • KIKAO CHA UCHUNGUZI WA TATHMINI YA ATHARI KWA MAZINGIRA NA JAMII WA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA LA AFRIKA MASHARIKI

    June 02, 2017
  • Siku ya uzinduzi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi wilaya ya Kilindi

    May 21, 2017
  • Tazama zote

Video

Mhe.Omary Kigua ataka ujenzi wa barabara za lami Kilindi
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Hati ya Mishahara
  • Mfumo wa Mpango na Bajeti
  • Mfumo wa ffars
  • Mwongozo wa Kutumia Mfumo wa FFARS
  • Taarifa kwa Umma

Tovuti Nyingine

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Baraza la Taifa la Elimu ya kiufundi
  • Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala bora
  • Tovuti ya Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

Visitors Counter

Acadooghostwriter.com

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.