• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kilindi District Council
Kilindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara/Vitengo
      • Idara
        • Elimu Msingi
        • Elimu Sekondari
        • Afya na Ustawi wa Jamii
        • Maendeleo ya Jamii
        • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Ardhi na Maliasili
        • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
        • Usafi na Mazingira
      • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Shughuli za Mifugo na Uvuvi
    • Shughuri za Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji na Umwagiliaji
    • Huduma za Kilimo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu na Majukumu yake
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao vya Kisheria
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Mradi wa Maji
      • Miradi ya Afya
    • Miradi inayoendelea
      • Huduma za Afya
      • Mradi wa Maji
    • Miradi iliyokamilika
      • Huduma za Afya
      • Mradi wa Maji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video Mbalimbali

Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika

IDARA YA KILIMO NA USHIRIKA

-Kuratibu huduma za kilimo za ugani ili kuboresha uzalishaji na kuzuia uharibifu wa mazingira.

•Kushirikiana na wadau wa kilimo kuanzisha mashamba darasa.

•Kutoa taarifa mbalimbali kuhusu mazao ya kilimo na masoko.

•Kutunza takwimu za uzalishaji wa mazao ya kilimo.

•Kutoa taarifa kuhusu usalama wa chakula katika wilaya.

•Kuwafundisha wakulima kuhusu kilimo bora na mbinu bora za kuhifadhi mazao.

-Kuratibu shughuli za ushirika.

•Kukagua hesabu za vyama vya Ushirika.

•Kusimamia Mikutano Mikuu ya vyama vya Ushirika.

•Kusajili Vyama vya Ushirika.

•Kukusanya takwimu za biashara ya mazao ya kilimo  katika vyama vya Ushirika.


KITENGO CHA USHIRIKA

1.0       UTANGULIZI

Ushirika ni kitengo ndani ya Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika. Nchini Tanzania Ushirika unaongozwa na Sheria ya Ushirika Namba 6 ya mwaka 2013 na Kanuni zake za mwaka 2015. Ushirika   huendeshwa   katika   misingi   saba   ya   Ushirika   inayotambulika   duniani   kote  na kuzingatia maadili  ya Ushirika  ambayo yalipitishwa  na Tamko la  Muungano wa  Vyama  vya Ushirika Duniani (International Co-operative Alliance – ICA) maadili hayo ni; Uanachama wa Hiari na ulio wazi, udhibiti wa Kidemokrasia/kiutawala, Ushiriki wa wanachama katika shughuli za kiuchumi, Uhuru na kujitegemea, Elimu, mafunzo na taarifa, Ushirika miongoni mwa  vyama vya ushirika na Ushirika kuijali jamii.

2.0       LENGO LA USHIRIKA

Lengo kuu la Ushirika ni kuinua kipato cha wanachama na jamii kwa ujumla, kuungana na kufanya kazi pamoja kwa hiari na kufanikisha mahitaji ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kupitia shughuli inayomilikiwa pamoja na kudhibitiwa kidemokrasia.

3.0       MAJUKUMU YA OFISI

Ofisi ya Ushirika inayo wajibu wa kutekeleza majukumu ya kisheria, usajili na kuwezesha udhibiti na usimamizi wa Vyama vya Ushirika katika Wilaya, ikiwa pamoja na kutekeleza majukumu yafuatayo;

  • Kuhamasisha uundwaji wa vyama vya Ushirika;
  • Kusimamia kuandikisha vyama vya Ushirika;
  • Kutoa mafunzo  ya uhasibu wa hesabu na kumbukumbu zote muhimu kwa watendaji wa vyama vya Ushirika;
  • Kufanya   ukaguzi   wa   mahesabu   na   kufuatilia   uendeshaji   wa   vyama   vya   Ushirika kulingana na sheria ya Ushirika;
  • Kuwezesha   tafsiri   ya   akaunti   zilizokaguliwa   na   mizania   kwa   ajili   ya     matumizi   ya wanachama katika vyama vya ushirika;
  • Kufanya uchunguzi na kuhoji hoja zinazoibuliwa katika vyama  vya msingi ushirika;
  • Kutoa Elimu ya Ushirika kwa wanachama na Viongozi wa vyama vya Ushirika;
  • Kukusanya na kutunza takwimu mbalimbali  za vyama vya Ushirika;
  • Kusimamia mikutano mikuu ya vyama vya Ushirika;
  • Kusimamia mikutano ya uchaguzi wa viongozi wa vyama vya Ushirika;
  • Kutekeleza Sheria ya vyama vya ushirika na kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika;

4.0       AINA YA VYAMA VYA USHIRIKA VILIVYOPO WILAYANI KILINDI

Ushirika hutofautiana kutokana na mahitaji ya jamii husika, kuna aina mbalimbali za Ushirika kama vile Ushirika wa kuweka na kukopa (SACCOS), Ushirika wa mazao (AMCOS), Ushirika wa viwanda, Ushirika wa madini na nyingine nyingi kutegemeana na mfungamano “common bond” ya jamii husika. Kuna aina mbalimbali za ushirika hapa Wilayani Kilindi kama vile Ushirika wa kuweka na kukopa (SACCOS), Ushirika wa mazao (AMCOS), Ushirika wa viwanda na Ushirika wa madini.

4.1       Ushirika  wa Akiba na Mikopo (SACCOS) 

SACCOS zilizopo Wilaya ya Kilindi ni pamoja na Umoja SACCOS, Kwamwande SACCOS, Baraka SACCOS, Azimio Mafisa Madukani SACCOS, Vijana SACCOS, Negero SACCOS, Muungano SACCOS, Kimbe SACCOS, Jaila SACCOS, Msanja SACCOS, Mafulila SACCOS, Kikunde SACCOS, Kilindi SACCOS, Songe Ward SACCOS, Songe Farmers and Business SACCOS na Kwediboma SACCOS.

 Madhumuni makubwa ya uwanzishwaji wa SACCOS hizo ni pamoja na :-

  1. Kuhamasisha wanachama wake kujenga tabia ya kujiwekea akiba mara kwa mara ;
  2. Kupokea na kutunza Hisa, Akiba na Amana za wanachama kwa njia rahisi na salama ;
  3. Kutafuta vyanzo vya fedha ili kujenga na kuimarisha mtaji kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanachama kwa masharti na riba nafuu ;
  4. Kuwaelimisha wanachama kujijengea tabia ya kukopa kwa busara na kutumia vizuri mikopo kwa ajili ya kuinua hali zao za maisha kiuchumi na kijamii ;
  5. Kutoa bidhaa mbalimbali za fedha (financial products) kwa wanachama ili waweze kushiriki zaidi kuimarisha mitaji ya chama na mitaji yao binafsi na kuleta mvuto kwa wasio wanachama kujiunga na chama ;
  6. Kuweka kwa usalama fedha za chama na wanachama kwa kuanzisha mipango ya kukabiliana na majanga na/au kuweka Bima za fedha zinazofaa ;
  7. Kuwashauri wanachama kuandaa mipango yao ya maendeleo katika kuwekeza mitaji kwenye miradi ya kiuchumi na huduma za jamii ;
  8. Kutoa elimu ya Ushirika kwa wanachama wake na wale wasio wanachama.

 

4.2       Ushirika wa Mazao (AMCOS)

AMCOS zilizopo wilayani Kilindi ni Nguu Farmers, Kilindi Farmers, Kilimo Mseto na Kingo Farmers.

Madhumuni ya uwanzishwaji wa vyama hivyo ni pamoja na:-

  1. Kuinua na kustawisha hali ya uchumi na maisha ya wanachama wake na hasa kuongeza pato la mwanachama kwa njia ya kuongeza uzalishaji/tija;
  2. Kuendeleza shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali kwa wanachama wake na ikiwezekana kuendeleza kilimo cha ushirika na shughuli nyingine za kiuchumi;
  3. Kuhifadhi kugawa/kuuza zana za kilimo, pembejeo, bidhaa muhimu na zana zote zitakazohitajika katika kuendeleza madhumuni ya chama kiuchumi;
  4. Kununua, kuendesha na kutunza mashine kwa ajili ya kusindika/kutengeneza mazao ya kilimo na mazao mengine;
  5. Kuanzisha na kuendesha mashamba makubwa;
  6. Kuwapatia wanachama wake ushauri juu ya kilimo bora cha mazao mengine;
  7. Kuendeleza na kutunza ardhi ambayo inaweza kugawiwa kwa wanachama kwa matumizi binafsi au kwa kilimo cha mazao.

4.3       Ushirika wa Kiwanda

Wilaya ya Kilindi ina chama kimoja cha Ushirika wa Kiwanda ambacho kinaitwa Kilindi Industrial Co-operative, madhumuni yake ni pamoja na:- 

  1. Kuwa na viwanda vya kusindika nafaka na mazao mengine yatokanayo na kilimo,  mifugo na maliasili kwa ajili ya kuuza;
  2. Kuendeleza na kupanua zana zake za uzalishaji ikiwa ni pamoja na malengo, huduma, mashine na vifaa vingine vinavyohusiana na biashara yake;
  3. Kutafuta, kununua na kuhifadhi malighafi na bidhaa nyingine zinazoweza kutumika viwandani;
  4. Kuzalisha/kutengeneza bidhaa za aina  mbalimbali kutokana na malighafi ya aina yeyote inayohusiana na shughuli husika kwa ajili ya kuuza au kwa mkataba.
  5. Kutafuta soko la bidhaa zitakazotengenezwa/kuzalishwa;
  6. Kuchunguza mara kwa mara mbinu za uzalishaji ili kuhakikisha kwamba ubora wa bidhaa unaimarishwa kufuatana na mahitaji ya masoko;
  7. Kutoa elimu ya Ushirika , stadi za biashara ya viwanda na kilimo cha kibiashara.

4.4       Ushirika wa Madini

Vilevile, wilaya ya Kilindi ina jumla ya vyama viwili vya Madini ambavyo ni pamoja na  Kiwaleke Mining Co-operative na Ngeze Mining Co-operative.

 Madhumuni  ya uwanzishwaji wake ni pamoja na:-

  1. Kutafuta Leseni kwa ajili ya utafiti wa madini na uchimbaji;
  2. Kupatia zana za uchimbaji wanachama kwa kuwauzia au kwa mkopo;
  3. Kutoa huduma za uongozi na uandaaji wa mikata kwa wanachama kwa ajili ya uendelezaji, utumiaji na uuzaji wa madini au mazao yatokanayo na madini;
  4. Kutafuta Kumiliki ardhi/viwanja vya machimbo kwa ajili ya wanachama;
  5. Kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira;
  6. Kumiliki zana kubwa za uchimbaji na kuzitunza kwa njia ya kuwakodisha wanachama.
  7. Kutoa elimu ya ushirika na stadi za biashara ya madini;
  8. Kuweka utaratibu wa upokeaji na uhifadhi wa madini kutoka kwa wanachama.

Imeandaliwa na,

Romana Milinga

KAIMU AFISA USHIRIKA (W)

Matangazo

  • NAMNA YA KUPATA KITAMBULISHO CHA MJASIRIAMALI KILINDI D-TANGA May 03, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KILINDI June 07, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA KILINDI YANUNUA KILO 3707 ZA MBEGU ZA MAHARAGWE KUPITIA MAPATO YA NDANI

    March 21, 2023
  • HALMASHAURI YA WILAYA KILINDI YANUNUA KILO 890 ZA MBEGU ZA ALIZETI KUPITIA MAPATO YA NDANI

    March 20, 2023
  • MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA KILINDI AMSHUKURU MH:RAIS KWA KUIPATIA HALMASHAURI PIKIPIKI

    March 20, 2023
  • MRADI WA UJENZI WA NYUMBA YA MADAKTARI WAKAMILIKA

    March 13, 2023
  • Tazama zote

Video

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda S.Mtondoo alipotembelea Mgodi wa Dhahabu wa Seita
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Hati ya Mishahara
  • SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO TANZANIA, 2015
  • SERA YA TEHAMA YA TAIFA YA MWAKA 2016
  • SHERIA YA MIAMALA YA KIELEKTRONIKI YA MWAKA 2015
  • SHERIA YA MAWASILIANO YA KIELEKTRONIKI NA POSTA 2010
  • KITENGO CHA MUITIKIO WA DHARURA WA MATUKIO YA MITANDAONI
  • Mfumo wa Mpango na Bajeti
  • Mfumo wa ffars
  • Mwongozo wa Kutumia Mfumo wa FFARS

Tovuti Nyingine

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Baraza la Taifa la Elimu ya kiufundi
  • Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala bora
  • Tovuti ya Ikulu
  • TUME YA TAIFA YA UKIMWI TANZANIA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.