Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilindi bwana Gracian Makota amemshukuru Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuipatia Halmashauri Pikipiki 6
Mkurugenzi Makota alisema Pikipiki hizo zitasaidia shughuli za serikali ikwemo ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri
Alisema Mh Rais Dk samia katika uongozi wake amekuwa akihakikisha kero za watumishi zinatatuliwa ikiwemo kuwapatia vitendea kazi vya usafiri na kuongeza kuwa Pikipiki hizo zimegawanywa kwa watendaji wa kata 6 ambazo zipo pembeni na mbali na makao makuu na kuagiza vyombo hivyo vitumike kwa ajili ya kazi za serikali
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kilindi Mh Idrisa Mgaza aliwataka watendaji kata watakaopatiwa Pikipiki hizo kuzitumia kwa maslahi ya serikali na atakayebainika kuzitumia vinginevyo atachukuliwa hatua kali za kisheria
Watendaji wa kata waliopatiwa Pikipiki hizo ni kutoka akata za Kilwa,Pagwi,Lwande,Saunyi,Mkindi na Negero
Modi Mngumi-Kilindi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.