Serikali imedhamiria kwa vitendo kufufua zao la Pamba ili kuinua uchumi wa wananchi wake ambao wengi ni wakulima.
Dhamira hiyo ya kufufua zao la Pamba imedhihirika wazi baada ya serikali kutoa kilo 3250 za mbegu za Pamba kwa Halmashauri ya wilaya Kilindi
Akizungumzia mbegu hizo mtaalamu wa kilimo katika Halmashauri ya wilaya Kilindi bwana Seifu Sempanga alisema kiasi hicho cha mbegu ambacho ni awamu ya kwanza tayari kimeshagawanywa kwa wakulima katika tarafa za Kimbe na Mswaki maeneo ambayo Pamba inastawi vizuri
Alisema kila kata imepata kilo 650 na katika tarafa ya Kimbe mbegu hizo zimetolewa katika kata ya Negero ambapo katika tarafa ya Mswaki zimetolewa katika kata ya Mkindi
Alisema lengo la serikali ni kuhakikisha kilimo cha Pamba kinafufuliwa na kuendelezwa ili wakulima waweze kunufaika
MWISHO
MODI MNGUMI-KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
HALMASHAURI YA WILAYA KILINDI
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.