Umoja wa wazazi na walimu (UWAWA) kupitia mradi wa Shule Bora umezaa matunda kwa watoto wa shule ya msingi Kwamazuma iliyopo kata ya Kilindi katika Halmashauri ya Wilaya Kilindi baada ya kufanikisha ujenzi wa tenki la maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali shuleni hapo.
Tenki hilo lenye ujazo wa lita 21,214.2 limejengwa kwa gharama za shilingi 1,921,000/= ambapo kati ya fedha hizo michango ya fedha taslimu ni shilingi 1,551,000/= na nguvu kazi ni 370,000/=
Shule ya Kwamazuma ina wanafunzi 517 kati yao wavulana ni 254 na wasichana ni 263 ambao hutembea umbali wa kilomita 6 kutafuta maji
Baada ya mafunzo ya UWAWA kupitia mradi wa Shule Bora ngazi ya wilaya yaliyofanyika tarehe 16-18/03/2023,wazazi na walimu katika shule ya msingi Kwamazuma walikaa tarehe 28/03/2023 kuutambulisha mradi, tarehe 04/04/2023 mradi ulipitishwa na kuanza rasmi tarehe 19/04/2023 ambapo kila mzazi mwenye mwanafunzi shuleni hapo alichanga fedha taslimu 3,000/=
Wakizungumzia mradi wa Shule Bora wazazi na wananchi mbalimbali wilayani Kilindi wametoa pongezi kwa mradi huo kwa kuijengea jamii uwezo na hatimaye kujua umuhimu wa kushiriki katika kutatua kero mbalimbali
Modi Mngumi
Mawasiliano Serikalini Kilindi Halmashauri ya wilaya Kilindi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.