Kumshauri Mkurugenzi wa Halmashauri kuhusu shughuli zote zinazohusu Idara ya Elimu ya Sekondari
Kusimamia mitihani yote ya ndani na ile ya Taifa yaani Mitihani ya kidato cha II,IV.VI na Vyuo vya Ualimu
Kusimamia, kuratibu na kufuatilia shughuli za ujenzi wa miundombinu katika shule za Sekondari kama vile nyumba za walimu, madarasa, majengo ya utawala, maabara, mkataba na vyoo
Kusimamia na kuratibu shughuli zote za Ukusanyaji, uchambuzi na kutafsiri takwimu za Idara ya elimu Sekondari na kuzituma kwa wadau wa elimu
Kusimamia na kuratibu shughuli za uandaaji wa taarifa na kuzituma kwa wadau mbalimbali wa elimu ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa
Kusimamia na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata taaluma kwa kiwango kilicho bora kwa mujibu wa Sera ya Elimu ya mwaka 1995 na 2014.
Kusimamia na kuhakikisha nidhamu ya wanafunzi, walimu na watumishi wasio walimu inadumishwa shuleni
Kusimamia na kuhakikisha fedha za Idara ya Elimu Sekondari zinatumika kwa kufuata kanuni, sheria, taratibu na miongozo ya fedha za Serekali za Mitaa
Kuhakikisha vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinapatikana katika shule za sekondari
Kuhakikisha kuwa shule zote za Sekondari zina samani za kutosha kwa ajili ya walimu na wanafunzi
Kuandaa ajenda na kuhudhuria vikao vyote vinavyohusu Idara ya Elimu Sekondari
Kuandaa taarifa za utekelezaji za Idara ya elimu sekondari za robo na mwaka na kuziwasilisha kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kama vile Waheshimiwa Madiwani, Mkoa na Taifa
Kuandaa makisio ya bajeti ya Idara ya Elimu ya Sekondari kila mwaka.
Kupokea na kuwapangia vituo walimu na wafanyakazi wa idara wanaohamia au wanaoajiriwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi